Tuesday, 31 March 2015

UTAFANYA NINI KAMA UKIJIKUTA UNAPENDA TENA WAKATI TAYARI UPO KWENYE MAHUSIANO NA MTU MWINGINE?



" moyo wangu ulishindwa kujizuia kabisa kila nikijaribu kuisahau habari yake
ilishindikana na tena moyo wangu uliguswa kwa nguvu zaidi hata ilivyokuwa nilipokutana na huyu mpenzi wangu wa sasa."
anasema Jack,
hali ya namna hii imekuwa ikiwatokea watu wengi sana , na asilimia kubwa kati yao
wamejikuta wakivuruga mahusiano yao ya awali sababu mahusiano hayo mapya.

lakini hilo ni jambo sahihi, uachane na mpenzi wako wa sasa eti sababu mtu mwingine ameusisimua moyo wako kwa ghafla?

"sijui kama nilikuwa sahihi lakini nilisikia sauti toka moyoni mwangu ikiniambia,
unamhitaji huyu Frenky huyu ndiye chaguo la moyo wako mwanzoni ulifanya makosa"
huyu ni frenky, lakini si Frenky pekee mwenye mawazo ya namna hii ,
pengine hata wewe ukikutana na hali kama hii ukajikuta ukiongozwa na mawazo ya namna hii.
sitaki kukueleza kwamba hauko sahihi ama uko sahihi ila nafikiri unatakiwa kujiuliza maswali haya:

NI KWELI UNAMPENDA?
hili ni swali rahisi sana lakini linaumuhimu sana katika hali kama hii, kwakuwa inawezekana ukavutiwa sana na muonekano wake na ukijikuta unafikiri unampenda.
Dr.Ray Short katika makala yake ya understanding True love anasema
" kabla haujamuoa msichana kwa sababu ya sura yake nzuri na umbile
lake lenye mvuto wa kimahaba jiulize mwenyewe kwanza msichana huyo atakuwaje miaka 30 ijayo?"

JE YEYE PIA ANAKUPENDA?
Usipofikiria juu ya suala hili ,hakika nakweleza hauwezi kuwa sahihi na maamuzi yako kwakuwa unaweza kuachana na mpenzi wako wa mwanzo kumbe mtu unaemuangaikia hana mapenzi ya kweli nawe, pengine amejisogeza kwako ili akutumie tu na kukuacha.

VIPI KUHUSU MPENZI WAKO WA AWALI?
je ni kweli hafai kiasi cha kustahili kuachwa , ni kweli pengo lake laweza kuzibwa na huyo Mpenzi wako wako wa sasa?
haya ni maswali ya msingi zaidi kujiuliza , usije ukafanya uamuzi ambao baadae ukakufanya ujutie maisha yako yote.

JAMII YAKO INALICHUKULIA VIPI SWALA HILI?
unaweza kufikiri hayo ni maisha yako hivyo huitaji kujua chochote kuhusu jamii yako katika maamuzi yako lakini mchango wa jamii yako katika kuchagua kilicho bora kwako ni muhimu zaidi ya hata wewe unavyofikiri, wao ni watu wako mara zote wanafikiri kile kilicho bora kwako.

Thursday, 26 March 2015

KWA NINI MOYO WAKO UUMIE UNAPOMUONA MPENZI WAKO WA ZAMANI AKIWA NA MPENZI WAKE MPYA?



unaweza kuwa katika hali ya furaha ukifurahi na marafiki zako huku mkipata kiburudisho fulani,
alafu ghafla furaha yako yote ikapotea , moyo wako ukajaa chuki na hasira za wivu.
hali hiyo usiyoitarajia inakukumba mara tu umuonapo mpenzi wako wa zamani akiwa na mpenzi wake mpya wakiponda raha.
Kwa nini siku yako iharibike hivi, unafikiri unastahili kupoteza furaha yako kwa sababu yao?
huenda usipate nafasi ya kujiuliza swali la namna hii, badala yake ukaamua kuondoka mahali hapo na kwenda sehemu nyingine ambayo ukadhani utenda kuirejesha furaha yako tena .
lakini hata hivyo utawakimbia mpaka lini, na unafikiri utakimbia umbali gani ili uepuke maumivu hayo yanayoupata moyo wako?
pengine utakuwa ulijui hili lakini usijali leo ntakueleza, hakuna umbali wowote katika dunia hii utakaokimbia na kukufanya usahau habari ya mpenzi wako wa zamani kama wewe mwenyewe hautakuwa tayari kusahau.
JIAMINI
lazima ukubali kwamba kuachana ni sehemu ya maisha na haimaanishi ukiachana na mpenzi wako hautoweza kusonga mbele.
Tambua kwamba maisha yako yanakuitaji wewe tu yeye alikuwa sehemu ya hadithi yako na nafasi yake imekwisha.

KWANINI NI VIGUMU KURUDISHA IMANI KWA MTU ALIYEKUSALITI?



" kuna kipindi huwa nailaumu nafsi yangu nikisema si yalikwisha na nilikwisha msamehe mbona simwamini tena?"
anasema Monica
si monica peke yake anaelalamikia jambo hili maelfu ya watu ulimwenguni kote wameshindwa kabisa kuwaamini tena wenzi wao walio wasaliti.
" kila anaponiambia naomba uniamini mpenzi mimi si yule wa mwanzo ni kama ananiambia kwamba sasa ndiyo naenda kukusaliti kwa kweli siwezi tena kumwamini"
anasema Abdalla.
huenda hata wewe ukajikuta katika hali ya namna hiyo hiyo ukikubwa na tatizo kama hili.

una fikiri ipo namna kurejesha imani yako tena?

' imani ni kitu kigumu zaidi kukirejesha na kinaitaji muda kukifanikisha. '
hivyo hupaswi kuilaumu nafsi yako , kuirudisha imani yako kunategemea sana vitendo vya mwenzi wako aliyekusaliti pamoja na kusamehe na kusahau yale aliyoyatenda.
kama yeye hatokuwa na bidii za kukushawishi wewe umwamini tena itakuwia vigumu sana wewe kurudisha imani kwake.
kama hatoonyesha ushirikiano wowote au pengine akaendeleza vitendo vyake vya usaliti kamwe huwezi kurudisha imani kwake
hata kama unampenda kiasi gani.


Wednesday, 25 March 2015

UTAFANYA NINI KAMA WEWE NA RAFIKI YAKO MMEMPENDA MTU MMOJA?



kila mtu ana haki ya kupenda , na kupendwa pia. 
na mara nyingi hali ya kumpenda mtu huja ghafla , mara tukigundua kwamba tumependa huwa tunafurahi na kujiona wenye bahati.
lakini vipi kama ukijikuta umempenda mtu ambaye rafiki yako amempenda pia?

" nilipomuona kwa mara ya kwanza tu nilijua kwamba huyu ndiye mwanaume wa ndoto yangu lakini kabla sijaongea jambo lolote Prisca aliniambia kwamba anampenda mwanaume huyo na asingeweza kuishi bila yeye na aliniomba ushauri afanye nini ili ampate
haikuwa taarifa nzuri kabisa kwangu nilitamani hata kumwongopea na kumweleza mwanaume huyo ni wangu lakini niliona isingefaa kwa kuwa hata yeye mwenyewe anajua kwamba sote ndio tunakutana na mwanaume huyo kwa mara ya kwanza."
Anita anasimulia.
" nisingeweza kuuvunja moyo wangu tena na wala nisingelifanya jambo la kuuvunja urafiki wangu wa muda mrefu sababu ya mapenzi pekee."
anazidi kusimulia ,
uenda wakati huu mgumu aliokumbana nao Anita hata wewe umewahi kukumbana nao katika kipindi fulani cha maisha yako.
ungeweza kukubali kuuvunja moyo wako ukitumaini utapata nafasi nyingine ya kupenda kama ambavyo Anita alifanya kwa upendo wa rafiki yake au ungefanya maamuzi yako binafsi?
vyovyote utakavyoamua lazima uzingatie haya

YEYE ANAMPENDA NANI?
Huwezi kuingia kwenye uhasama na rafiki yako au kuamua jambo lolote kama ujaujua msimamo wa mtu huyo, pengine hana mpango na yoyote 
kati yenu mwisho mnaishia kulumbana pasipo faida yoyote.

VIPI KUHUSU RAFIKI YAKO?
je anamapenzi ya kweli kama wewe au anampenda kwa sababu fulani. unaweza ukamuachia nafasi hiyo rafiki yako alafu mwisho wa siku nae pia akaipoteza kwa kuwa hakuwa na malengo nae.

ONGEA NA RAFIKI YAKO
mweleze hali halisi rafiki yako na mjadiliane pasipo malumbano ili kulinda urafiki wenu mkubaliane kabisa nani anastahili nafasi hiyo na kamwe maongezi yenu yasiishie katika malumbano au uhasama kila mmoja alithike na makubaliano yenu.