UTAFANYA NINI KAMA UKIJIKUTA UNAPENDA TENA WAKATI TAYARI UPO KWENYE MAHUSIANO NA MTU MWINGINE?
" moyo wangu ulishindwa kujizuia kabisa kila nikijaribu kuisahau habari yake
ilishindikana na tena moyo wangu uliguswa kwa nguvu zaidi hata ilivyokuwa nilipokutana na huyu mpenzi wangu wa sasa."
anasema Jack,
hali ya namna hii imekuwa ikiwatokea watu wengi sana , na asilimia kubwa kati yao
wamejikuta wakivuruga mahusiano yao ya awali sababu mahusiano hayo mapya.
lakini hilo ni jambo sahihi, uachane na mpenzi wako wa sasa eti sababu mtu mwingine ameusisimua moyo wako kwa ghafla?
"sijui kama nilikuwa sahihi lakini nilisikia sauti toka moyoni mwangu ikiniambia,
unamhitaji huyu Frenky huyu ndiye chaguo la moyo wako mwanzoni ulifanya makosa"
huyu ni frenky, lakini si Frenky pekee mwenye mawazo ya namna hii ,
pengine hata wewe ukikutana na hali kama hii ukajikuta ukiongozwa na mawazo ya namna hii.
sitaki kukueleza kwamba hauko sahihi ama uko sahihi ila nafikiri unatakiwa kujiuliza maswali haya:
NI KWELI UNAMPENDA?
hili ni swali rahisi sana lakini linaumuhimu sana katika hali kama hii, kwakuwa inawezekana ukavutiwa sana na muonekano wake na ukijikuta unafikiri unampenda.
Dr.Ray Short katika makala yake ya understanding True love anasema
" kabla haujamuoa msichana kwa sababu ya sura yake nzuri na umbile
lake lenye mvuto wa kimahaba jiulize mwenyewe kwanza msichana huyo atakuwaje miaka 30 ijayo?"
JE YEYE PIA ANAKUPENDA?
Usipofikiria juu ya suala hili ,hakika nakweleza hauwezi kuwa sahihi na maamuzi yako kwakuwa unaweza kuachana na mpenzi wako wa mwanzo kumbe mtu unaemuangaikia hana mapenzi ya kweli nawe, pengine amejisogeza kwako ili akutumie tu na kukuacha.
VIPI KUHUSU MPENZI WAKO WA AWALI?
je ni kweli hafai kiasi cha kustahili kuachwa , ni kweli pengo lake laweza kuzibwa na huyo Mpenzi wako wako wa sasa?
haya ni maswali ya msingi zaidi kujiuliza , usije ukafanya uamuzi ambao baadae ukakufanya ujutie maisha yako yote.
JAMII YAKO INALICHUKULIA VIPI SWALA HILI?
unaweza kufikiri hayo ni maisha yako hivyo huitaji kujua chochote kuhusu jamii yako katika maamuzi yako lakini mchango wa jamii yako katika kuchagua kilicho bora kwako ni muhimu zaidi ya hata wewe unavyofikiri, wao ni watu wako mara zote wanafikiri kile kilicho bora kwako.
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home