Sunday, 12 April 2015

UNAFIKIRI UNAHITAJI KUYACHUKIA MAPENZI UKIVUNJWA MOYO NA MPENZI MLIOACHANA?


Hakuna anaetarajia maumivu mara tu anapoanzisha mahusiano ya kimapenzi , badala yake tunatarajia furaha lakini ajabu waliowengi wanajikuta wanakutana na maumivu makali ya moyo hata kujikuta wanayachukia mapenzi na kujichukia wenyewe wakijiona hawafai.



KWANINI UYACHUKIE MAPENZI SABABU MTU MMOJA PEKE YAKE?



najua jinsi ulivyokuwa umeuwekeza moyo wako kwake , na ni jinsi gani inavyouma ukivujwa moyo na mtu uliyempenda  sana .

 lakini kosa lake halimaanishi kwamba watu wote wa jinsia yake wanatabia kama zake , hata kama umekutana na wengi wa aina hiyo na wote wakakuumiza moyo kama alivyofanya yeye bado hautakiwi kuvunjika moyo wala kuyachukia mapenzi.
kumpata anaekupenda kwa dhati ni kazi na mungu pekee ndio anajua ni yupi hasa mwenye mapenzi ya kweli.
na lazima atakufikia siku moja na atasema inatosha , kamwe hatoruhusu chozi lisilo la furaha lidondoke kwenye mashavu yako.
lakini unahitaji kuomba mungu.